Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Sharti ya nne ni mtu kuondosha hadathi, nako ni kule kutia wudhuu´ unaojulikana.

MAELEZO

Maneno yake matunzi:

“Sharti ya nne… “

Miongoni mwa sharti za kusihi kwa swalah ni kuondosha hadathi. Nako ni kule kutia wudhuu´ unaojulikana. Kwa msemo mwingine ni lazima mtu atawadhe ili aweze kuswali.

Hadathi ni kitu cha kimaana anachokifanya mtu kikamzuia kuswali, kugusa msahafu, kutufu Ka´bah na kadhalika. Hadathi sio najisi. Najisi inapogusa nguo au mwili inaoshwa  na sehemu hiyo panasafika. Hadathi, kama vile kinyesi, mkojo au upepo kutoka kupitia njia ya mbele au ya nyuma, kugusa tupu kwa mkono, kula nyama ya ngamia na mengineyo kama yatavyokuja katika maneno ya mtunzi (Rahimahu Allaah) kuhusu vichenguzi vya wudhuu´.

Mtu akipatwa na kitu katika vile vinavyochengua wudhuu´ ndio huitwa ´hadathi`. Ni lazima  aondoshe hadathi hii kwa kutawadha. Hiyo ni sharti miongoni mwa sharti za swalah. Asiyeondosha hadathi ambapo akatawadha, basi ni mwenye hadathi na swalah yake ni batili haisihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 07/12/2021