09. Hadiyth ”Nilimuona Mtume akiswali… ”

al-Bayhaqiy (2/420) amesema: Abu Bakr bin al-Haarith al-Faqiyh ametufahamisha: Abu Muhammad bin Hayyaan ametufahamisha: ´Aliy bin Sa´iyd ametuhadithia: Muhammad bin Sinaan al-Qazzaaz[1] ametuhadithia: Abu Ghassaan al-´Anbariy ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa Humayd bin Hilaal, kutoka kwa ´Abdullaah bin as-Saamit, kutoka kwa Abu Dharr, ambaye ameeleza:

”Nilimuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiswali akiwa na viatu vilivyotengenezwa kwa ngozi ya ng’ombe.”

al-Bayhaqiy amesema:

”Kutokana na ninavyojua Hadiyth hii imesimuliwa na Abu Ghassaan Yahyaa bin Kathiyr al-´Anbariy.”

[1] Muhammad bin Sinaan al-Qazzaaz ametajwa kuwa ni dhaifu katika “Taqriyb-ut-Taqriyb”.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 11-112
  • Imechapishwa: 01/06/2025