213 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لقد أُمِرتُ بالسواكِ حتى ظَنَنْتُ أنه يَنْزل عليَّ فيه قرآنٌ أو وَحيٌ

“Niliamrishwa kutumia Siwaak mpaka nikafikiri kuwa nitateremshiwa Qur-aan au Wahy juu yake.”[1]

Ameipokea Abu Ya´laa na Ahmad kwa tamko lisemalo:

لقد أُمِرتُ بالسواكِ حتى خَشيتُ أن يُوحَى إليَّ فيه شيء

“Niliamrishwa kutumia Siwaak mpaka nikachelea nitafunuliwa kitu juu yake.”

Wapokezi wake ni wenye kuaminika.

[1] Nzuri kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/204)
  • Imechapishwa: 13/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy