9- Muhammad bin al-Fadhwl bin Muhamamd at-Twaa-iy ametuhadithia: Muhammad bin ´Adiy bin Hamduuyah as-Swaabuuniy ametuhadithia: Abuul-Hasan bin Bashiyr ametuhadithia: Kaamil al-Muqriy ametuhadithia: Abuu ´Awaanah ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin ´Umayr, kutoka kwa Warraad, mwandishi wa al-Mughiyrah, kutoka kwa al-Mughiyrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:

“Sa´d bin ´Ubaadah amesema: “Iwapo ningemuona mwanaume pamoja na mke wangu basi ningelimpiga upanga kwa sababu ya wivu nilio nao.” Hayo yakamfikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasema: “Je, mnashangazwa na wivu wa Sa´d?” Ninaapa kwa Allaah kuwa nina wivu zaidi yake na Allaah ana wivu zaidi yangu. Kwa sababu ya wivu Wake ameharamisha machafu yaliyo dhahiri na yaliyofichikana. Hakuna shakhsw/kitu kilicho na wivu kama Allaah (´Azza wa Jall). Hakuna shakhsw/kitu kinachopenda udhuru kama Allaah (´Azza wa Jall). Kwa ajili hiyo katuma Mitume ili kuja kufikisha bishara njema na kuonya. Hakuna shakhsw/kitu kinachopenda kusifiwa kama Allaah (´Azza wa Jall).”[1]

[1] al-Bukhaariy (7417).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 30
  • Imechapishwa: 14/01/2017