23 – al-Hasan bin al-Husayn an-Ni´aaliy ametukhabarisha: Ahmad bin Naswr adh-Dhiraa´ ametukhabarisha huko Nahrawaan: Abul-Hasan ´Aliy bin Nasruuyah amenihadithia: Nimemsikia Husayn bin Bishr akisema: Nimemsikia Sahl bin ´Abdillaah akisema:

”Elimu ni moja katika starehe za dunia. Inapofanyiwa kazi inakuwa kwa ajili ya Aakhirah.”

24 – Abul-Qaasim ´Abdul-Kariym bin Hawaazin al-Qushayriy an-Naysaabuuriy ametukhabarisha: Nimemsikia Muhammad bin al-Husayn as-Sulamiy: Nimemsikia Abu Bakr ar-Raaziy: Nimemsikia al-Khawwaas akisema:

”Elimu sio kwa masimulizi mengi. Mwanachuoni ni yule mwenye kuifuata elimu na akaifanyia kazi na akafuata Sunnah, ingawa atakuwa na elimu chache.”

25 – Abu Hafsw ´Umar bin Muhammad bin ´Aliy bin ´Atwiyyah al-Makkiy ametukhabarisha: Abul-Fath Yuusuf bin ´Umar bin Masruur al-Qawwaas ametuhadithia: Ahmad bin ´Aliy ametuhadithia: Ziyaad bin Ayyuub ametuhadithia: Ahmad bin Abiyl-Hawaariy ametuhadithia: ´Abbaas bin Ahmad amenihadithia kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا

“Na wale waliofanya juhudi kwa ajili Yetu, bila shaka tutawaongoza njia Zetu.”[1]

”Bi maana wale wanaofanyia kazi yale waliyojifunza; Tutawaongoza katika yale wasiyoyajua.”

26 – Abul-Husayn Ahmad bin ´Aliy bin al-Husayn at-Tuuziy ametukhabarisha: Abu ´Abdir-Rahmaan Muhammad bin al-Husayn an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Nimemsikia Abu Bakr ar-Raaziy: Nimemsikia Yuusuf bin al-Husayn akisema:

”Ulimwenguni kuna mambo mawili ya kuchupa mpaka: uchupaji wa kwanza ni wa elimu na uchupaji mwingine ni wa mali. Kinachokuokoa dhidi ya uchupaji mipaka wa elimu ni ´ibaadah, na kinachokuokoa dhidi ya uchupaji mipaka wa mali ni kuzipa kinyongo.”

27 – Yuusuf amesema:

”Kwa adabu ndio utaifahamu elimu. Kwa elimu ndio utayarekebisha matendo yako. Kwa matendo ndio utafikia hekima. Kwa hekima ndio utafahamu na kuwafikishwa kunako kuipa kisogo dunia. Utaiacha dunia kwa kuipa kisogo. Kwa kuiacha dunia ndio utatamani Aakhirah. Kwa kutamani Aakhira ndio utapata radhi za Allaah (´Azza wa Jall).”

28 – Muhammad bin al-Husayn bin Muhammad al-Mattuuthiy amenikhabarisha: Ja´far bin Muhammad al-Khuldiy ametaja kwamba Abul-´Abbaas al-Hulwaaniy amemukhabarisha: Nimemsikia Abul-Qaasim al-Junayd akisema:

”Unapotaka kujitukuza kwa elimu, kujinasibisha nayo na kuwa miongoni mwa wenye nayo kabla ya kupewa elimu stahiki, nuru yake inazuiwa kutoka kwako na inabaki inaonekana kwako. Elimu hiyo inakuwa dhidi yako na si kwa ajili ya manufaa yako. Kwa sababu elimu inaashiria kuitumia. Elimu isipofanyiwa kazi katika viwango vyake, basi inaondoka ile baraka yake.”

[1] 29:69

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 29-31
  • Imechapishwa: 08/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy