Ikiwa mambo ni kama ulivoyajua, lakini pia kuna mengi zaidi ya tunayoyajua, kuwa ni mwenye tahadhari kubwa na ufisadi wa Usaamah bin Laadin na wasaidizi wake tuliyotangulia kuwataja. Kuwa ni mwenye tahadhari kubwa kuwajengea dhana nzuri au kueneza haraka zao. Hakika ya harakati zao zinafanywa katika njia ya Shaytwaan hata kama watadai kuwa ni katika njia ya Allaah. Kinaika ya kwamba wanatetea batili na ufisadi na sio wema na Jihaad. Batili ni ujasiri. Baada ya muda inaanguka na kupotea ilihali watu wake wanafikwa na khasira za Allaah ikiwa hawakutubu kwa Allaah na kujirudi katika nafsi zao katika maisha yao yaliyobaki. Allaah (Ta´ala) Amesema:

فَأَمَّا الزَّبَدُ فَيَذْهَبُ جُفَاءً ۖ وَأَمَّا مَا يَنفَعُ النَّاسَ فَيَمْكُثُ فِي الْأَرْضِ ۚكَذَٰلِكَ يَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ

“Basi povu linapita kama takataka [halifai chochote]. Lakini vile vinavyowafaa watu hubakia ardhini. Hivyo ndivyo Allaah anavyopiga mifano.” (13:17)

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Waqafaat wa Ma´aalim, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 13/01/2015