08. Hadiyth “Daku yote ni baraka… “

1070- Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Daku yote ni baraka. Hivyo msiiache ijapo mmoja wenu atakunywa glasi moja ya maji. Allaah (´Azza wa Jall) anawasifu na Malaika wanawaombea du´aa wale wenye kula daku.”[1]

Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi yenye nguvu.

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/620)
  • Imechapishwa: 23/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy