690- Aws bin Aws ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Atakayejitwaharisha[1] na kuoga siku ya ijumaa, akaenda kwa muda na mapema, akatembea na asipande, akawa karibu na imamu, akasikiliza na asifanye upuuzi, basi hulipwa kwa kila hatua moja ujira wa swawm ya mwaka mzima na kisimamo chake cha usiku.”[2]

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Hadiyth ni nzuri.”

Vilevile ameipokea an-Nasaa´iy, Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake, Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake na al-Haakim ambaye ameisahihisha.

[1] Katika Abu Daawuud imekuja:

”Atakayejitwaharisha kichwa chake.”

Mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh, kama ilivyotajwa katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (373). Haya yanatilia nguvu tafsiri ya Ibn Khuzaymah juu ya Hadiyth hii itayokuja kutajwa na mwandishi.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/433)
  • Imechapishwa: 10/03/2017