07. Wanachuoni waliyomnasihi Ibn Laadin na Genge lake

Wanachuoni wakubwa Saudi Arabia akiwepo kwenye ncha yao Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz na Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn (Rahimahumaa Allaah), Shaykh Swaalih al-Luhaydaan, Shaykh Swaalih al-Fawzaan, muftiy wa Saudi Arabia Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh na wengine wengi walimnasihi Usaamah bin Laadin na kundi lake, kuwatisha na adhabu ya Allaah na kuwausia kurudi katika haki na kuachana na batili yao ambayo madhara na shari yake imezunguka na kuenea. Pamoja na hivyo wenye chuki hawakuitikia. Hawakuitikia nasaha zao mpaka hii leo.

Ni mara ngapi wanachuoni hawa watukufu wametahadharisha faksi, tovuti kwenye intaneti, na vipindi vya redioni vya al-Mas´ariy, Sa´d al-Faqiyh na watu mfano wao na mikanda ya Ibn Laadin kutokana na mgawanyiko ilio nayo, mapinduzi dhidi ya watawala na matusi kwa wanachuoni wenye kutoa nasaha na mengine yasiyokuwa salama, yenye kuharibu na njia nyinginezo chafu zenye kutoka Uingereza – ambapo anaishi al-Mas´ariy na Sa´d al-Faqiyh – na mapango ya Afghanistan – ambapo Ibn Laadin anaishi – yanayopelekea na vita haribifu na yenye kusifidi ya kilimwengu ikianzia Saudi Arabia?

Matendo ya wanachuoni bila ya shaka ni katika kuamrisha mema na kukataza maovu, rehema kwa viumbe wa kuutakia Ummah yaliyo mazuri.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Waqafaat wa Ma´aalim, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 16/12/2014