07. Usitilie shaka imani yako

26 – Abu Usaamah ametuhadithia, kutoka kwa Mis´ar, kutoka kwa ´Atwaa’ bin as-Saa-ib, kutoka kwa Abu ´Abdir-Rahmaan ambaye amesema:

“Mmoja wenu akiulizwa kama ni muumini, basi asitie shaka.”

27 – Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Mis´ar, kutoka kwa Ziyaad bin ´Ilaaqah, kutoka kwa ´Ubaydullâh bin Ziyaad ambaye amesema:

“Akiulizwa mmoja wenu kama ni muumini, basi asitie shaka katika imani yake.”

28 – Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Mis´ar, kutoka kwa Muusa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa mtu ambaye hakumtaja jina, kutoka kwa baba yake ambaye ameeleza kuwa Ibn Mas´uud amesema:

“Mimi ni muumini.”

29 – Ibn Mahdiy ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa Ibn Twaawuus, kutoka kwa baba yake, na kutoka kwa Muhammad, kutoka kwa Ibraahiym aliyesema:

“Walipokuwa wanaulizwa kama ni waumini, basi husema: “Tunamwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Yake.”

30 – Abu Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa ash-Shaybaaniy aliyesema:

“Nilikutana na ´Abdullaah bin Mughaffal na nikasema: “Kuna watu wema wanaonikemea mimi kusema kuwa ni muumini.” Ndipo ´Abdullaah bin Mughaffal akasema: “Umeangamia na kukhasirika usipokuwa muumini.”

31 – Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa ´Umar bin Munabbih, kutoka kwa Sawwaar bin Shabiyb ambaye amesema:

“Bwana mmoja alikuja kwa Ibn ´Umar akasema: “Hapa kuna watu wanaonituhumu ukafiri.” Akasema: “Husemi ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` ukawakadhibisha?”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. ´Umar bin Munabbih na Sawwaar bin Shabiyb ni waaminifu. Ibn Abiy Haatim ametaja nyasifu zao katika  ”al-Jarh wat-Ta´diyl” (3/135) pamoja na (2/1/270).

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 22
  • Imechapishwa: 09/07/2023