7 – Siasa

Qur-aan imebainisha misingi yake, kuangazia alama zake na kuweka wazi njia zake. Kuna sampuli mbili za siasa: ya nje na ya ndani.

Kuhusu siasa ya nje, ni yenye kuzunguka katika misingi miwili:

1 – Kuandaa nguvu ya kutosha ili kujiweka tayari na adui. Amesema (Ta´ala) kuhusu msingi huu:

وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّـهِ وَعَدُوَّكُمْ

“Na waandalieni nguvu zozote mziwezazo na farasi waliofungwa tayari [kwa vita] muwaogopeshe kwayo maadui wa Allaah na maadui zenu.”[1]

2 – Umoja sahihi na wenye kuenea kwa ajili ya nguvu hiyo. Amesema (Ta´ala):

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

“Shikamaneni nyote pamoja kwa kamba ya Allaah na wala msifarikiane.”[2]

وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ

“Na wala msizozane, mtavunjikwa moyo na zikatoweka nguvu zenu.”[3]

Qur-aan imebainisha yenye kufuatia hayo katika kufanya mkataba wa amani na kuvunja mkataba mambo yakipelekea kufanya hivo. Amesema (Ta´ala):

فَأَتِمُّوا إِلَيْهِمْ عَهْدَهُمْ إِلَىٰ مُدَّتِهِمْ

“Watimizieni ahadi yao mpaka muda wao [utimie].”[4]

فَمَا اسْتَقَامُوا لَكُمْ فَاسْتَقِيمُوا لَهُمْ

“Wakikunyokeeni [kwa uzuri], nanyi wanyokeeni [kwa uzuri].”[5]

وَإِمَّا تَخَافَنَّ مِن قَوْمٍ خِيَانَةً فَانبِذْ إِلَيْهِمْ عَلَىٰ سَوَاءٍ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْخَائِنِينَ

“Na kama ukihofu khiyana kwa watu [mliofanya nao ahadi], basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Allaah hapendi makhaini.”[6]

وَأَذَانٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى النَّاسِ يَوْمَ الْحَجِّ الْأَكْبَرِ أَنَّ اللَّـهَ بَرِيءٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ ۙ وَرَسُولُهُ

“Na ni tangazo kutoka kwa Allaah na Mtume Wake kwa watu siku ya Hajj kubwa kwamba: Allaah na Mtume Wake wamejitenga mbali na washirikina.”[7]

Vilevile Ameamrisha kuwa makini na kujihadhari na njama zao na kutumia kwao fursa mbiombio wakipata namna ya kufanya hivo:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا خُذُوا حِذْرَكُمْ

“Enyi mlioamini! Chukueni tahadhari.”[8]

وَلْيَأْخُذُوا حِذْرَهُمْ وَأَسْلِحَتَهُمْ

“… nao washike hadhari na silaha zao.”[9]

Kuhusu siasa ya ndani, mambo yake yanarejea katika kueneza amani na utulivu ndani ya jamii, kuzima dhuluma zote na kumpa kila mmoja haki yake. Siasa ya ndani imejengwa juu ya nukta sita kubwa:

1 – Dini. Shari´ah imekuja kuhifadhi suala hili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kubadilisha dini yake muueni.”[10]

Hapo kuna matishio makali kwa yule mwenye kutaka kuibadilisha dini yake.

2 – Nafsi. Ili kuilinda nafsi, Allaah ameweka kisasi katika Kitabu Chake:

وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ

“Na mtapata katika [kulipiza] kisasi uhai.”[11]

كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى

“Mmewekewa Shari´ah kulipa kisasi katika waliouawa.”[12]

وَمَن قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا

“Na atakayeuliwa kwa kudhulumiwa, basi Tumemfanya msimamizi wake awe na mamlaka.”[13]

3 – Akili. Qur-aan imeteremsha mambo yenye kuihifadhi akili. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

“Enyi mlioamini! Hakika ulevi na kamari na [kuabudu] masanamu, na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli – vyote hivyo ni uchafu katika matendo ya shaytwaan. Basi jiepusheni navyo mpate kufaulu.”[14]

Katika Hadiyth imekuja:

“Kila chenye kulevya ni haramu. Ikiwa kiwango kikubwa kinalewesha, basi kiwango chake kichache pia ni haramu.”[15]

Kwa ajili ya kuihifadhi akili, ni wajibu kumuadhibu mwenye kunywa pombe.

4 – Nasaba. Kwa ajili ya kuihifadhi, Allaah ameweka adhabu kwa ajili ya uzinzi:

الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ

“Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamme, mpigeni kila mmoja katika wao mijeledi mia.”[16]

5 – Heshima. Kwa ajili ya kulinda heshima, Allaah ameweka ya kwamba yule mwenye kumtuhumu kwa uongo mtu uzinzi apigwe bakora themanini:

وَالَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَأْتُوا بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ فَاجْلِدُوهُمْ ثَمَانِينَ جَلْدَةً

“Na wale wanaowasingizia wanawake watwaharifu [kuwa wamezini] kisha hawaleti mashahidi wanne, basi wapigeni mijeledi themanini.”[17]

6 – Mali. Kwa ajili ya kuilinda, Allaah ameweka Shari´ah ya kukata mkono wa mwizi:

وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِّنَ اللَّـهِ

“Mwizi mwanamume na mwizi mwanamke wakateni mikono yao – ni malipo kwa yale waliyoyachuma; ndio adhabu ya mfano kutoka kwa Allaah.”[18]

Mpaka hapa inapata kubainika waziwazi ya kwamba Qur-aan inaidhamini jamii kwa manufaa yake yote, ni mamoja manufaa ya ndani na ya nje ya nchi.

[1] 08:60

[2] 03:103

[3] 08:46

[4] 09:04

[5] 09:07

[6] 08:58

[7] 09:03

[8] 04:71

[9] 04:102

[10] al-Bukhaariy (4/21).

[11] 02:179

[12] 02:178

[13] 17:33

[14] 05:90

[15] Ibn Maajah (2/1124). Kuhusu sehemu yake ya kwanza ”Kila chenye kulevya ni haramu”, iko katika al-Bukhaariy (5/108) na Muslim (3/1585).

[16] 24:02

[17] 24:04

[18] 05:38

  • Mhusika: Imaam Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Islaam diyn al-Kaamil, uk. 19-21
  • Imechapishwa: 13/06/2023