3 – Kulazimishwa kuolewa

Wakati mwingine msichana anakuwa amelazimishwa na baba yake au ndugu zake. Ni mamoja amelazimishwa kuolewa na mabinamu zake. Mara nyingi kulazimishana kuolewa inakuwa ni baina ya wale ndugu wa karibu na kulazimishwa inakuwa kwa yule wanayemtaka ilihali mwanamke yeye hamtaki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefanya msichana bikira kuolewa baada ya idhini na mwanamke ambaye kishawahi kuolewa kuamrishwa na akaeleza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoa kwake idhini ni kule kunyamaza kwake[1]. Kwa hivyo asilazimishwe mwanamke, ni mamoja ni bikira wala mwanamke ambaye kishawahi kuolewa. Vilevile mwanaume asilazimishwe. Ikiwa mwanamke halazimishwi basi mwanaume ana haki zaidi ya kutolazimishwa.

Baadhi ya watu wana kasumba za kipindi kabla ya kuja Uislamu. Wanawalazimisha watoto wao kuwaoa wasichana kadhaa kukiwemo mabinamu ilihali wao hawawataki wasichana hao. Matokeo yake wanawaoa shingo upande na wanaeshi muda autakao Allaah na hatimaye kunatokea talaka. Haya yanatokea katika jamii kadhaa. Nasema kuwa ni ´jamii za kipindi kabla ya kuja Uislamu`, nakusudia kipindi kabla ya kuja Uislamu kuhusu mambo ya Shari´ah, na sikusudii kipindi kabla ya kuja Uislamu kuhusu ukafiri.

[1] al-Bukhaariy (5136) na Muslim (1419).

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 31/03/2024