07. Moto unasubiri upande wa pili

Hapana shaka yoyote kwamba mwongo mwenye chongo atajitokeza. Yeye ndiye mwongo mkubwa kabisa.

Adhabu ndani ya kaburi ni haki. Humo mja ataulizwa juu ya Mola wake, Mtume wake na dini yake. Baada ya hapo ataona mahali pake Peponi au Motoni.

Munkar na Nakiyr ni haki. Wao ndio wenye kutoa mtihani ndani ya kaburi. Tunamuomba Allaah uthabiti.

Hodhi ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni haki. Wataiendea Ummah wake. Inayo vikombe ambavyo Ummah wake watakunywa ndani yake.

Njia ni haki. Itawekwa juu ya Moto. Watu watapita juu yake. Upande wa pili Pepo inawasubiri. Tunamwomba Allaah usalama na kuweza kuvuka.

Mizani ni haki. Mema na maovu yatapimwa kama Allaah atakavo yapimwe.

Baragumu ni haki. Israafiyl atapuliza ndani yake na wafe viumbe wote. Halafu atapuliza kwa mara nyingine ambapo watasimama mbele ya Mola wa walimwengu kwa ajili ya kufanyiwa hesabu na kuhukumiwa. Baada ya hapo wanasubiriwa ima na malipo au adhabu,  ima Pepo au Moto.

Ubao uliohifadhiwa ni haki. Kutokana vile mipango na makadirio vyote vimeandikwa humo, basi waja wanatenda kwa mujibu wa yaliyomo ndani.

Kalamu ni haki. Allaah ameandika kwayo makadirio ya kila kitu na ameyadhibiti kwa hesabu. Amebarikika Allaah (Ta´ala)!

Uombezi siku ya Qiyaamah ni haki. Kuna watu watawaombea watu wengine ili wasiingie ndani ya Moto. Wako watu ambao watatoka nje ya Moto baada ya wao kuingia kutokana na uombezi wa waombezi. Wako watu wengine wataotoka nje ya Moto kutokana na rehema za Allaah baada ya kuchomwa ndani yake kwa muda anaotaka Allaah. Kuna watu wengine ambao watadumishwa ndani ya Moto milele. Hawa ni wale washirikina, wakadhibishaji, wakanushaji na wenye kumkufuru Allaah (´Azza wa Jall).

Kifo kitachinjwa siku ya Qiyaamah kati ya Pepo na Moto.

Pepo tayari imeshaumbwa na vyote vilivomo ndani. Moto tayari umeshaumbwa na vyote vilivomo ndani. Allaah (´Azza wa Jall) aliviumba mwanzo kisha akaviumbia watu wake. Havitotokomea wala havitotokomea vilivyomo ndani yake.

Mzushi na zandiki akijengea hoja maneno ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala):

كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

“Kila kitu ni chenye kuangamia isipokuwa uso Wake.”[1]

na Aayah nyenginezo zisizo wazi, basi unatakiwa kumwambia kuwa Aayah inakusudia vile vyote ambavo Allaah ameviandikia kuteketea na kumalizika. Pepo na Moto vimeumbwa kwa ajili ya kubaki, na si kwa ya kuteketea na kumalizika. Aidha vitu hivyo ni katika Aakhirah na si katika dunia.

Huur-ul-´Ayn hawatokufa wakati wa kusimama kwa Saa wala wakati wa kupulizwa bagarumu. Kamwe hawafi. Kwa sababu Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amewaumba ili wabaki, na si kwa ajili ya kuteketea. Hakuwakadiria kufa. Ambaye atasema kinyume na hivo ni mzushi.

[1] 28:88

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 49-54
  • Imechapishwa: 25/05/2022