07 – Fadhilah za kumtaja Allaah
Tambua – ee msichana wa Uislamu – ya kwamba jambo bora zaidi mtu anaweza kujishughulisha wakati wake ni kumtaja Allaah, kumuomba, kumuomba msamaha na kusoma Qur-aan Tukufu. Hayo yanafanywa baada ya kutekeleza ´ibaadah za faradhi. Amesema (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا
“Enyi walioamini! Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru na msabihini asubuhi na jioni.”[1]
Imaam Ahmad amesimulia katika ”Musnad” yake ya kwamba kuna bwana mmoja ambaye alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Shari´ah za Kiislamu zimenilemea. Nieleze juu ya jambo ambalo nitajishughulisha nalo.” Akamjibu: ”Usiache ulimi wako kuwa na unyevunyevu kwa kumtaja Allaah.”
Ameipokea Imaam Ahmad, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah.
Miongoni mwa hayo ni Tasbiyh na Tahliyl. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kuna maneno mawili mepesi zaidi kwenye ulimi, mazito zaidi kwenye mizani na ni yenye kupendeza zaidi kwa Mwingi wa huruma:
سُبْحَانَ اللَّهِ ، وبِحَمْدِهِ سُبْحَانَ اللَّهِ الْعَظِيمِ
“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na sifa zote njema ni Zake. Allaah, hali ya kuwa ametukuka, ametakasika kutokamana na mapungufu.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ni manne:
سبحان الله، والحمد لله، ولا إله إلا الله، والله أكبر
”Allaah ametakasika na mapungufu, himdi zote njema anastahiki Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na Allaah ni Mkubwa.”
Haijalishi umeanza na yepi.”
Ameipokea Muslim.
[1] 33:41-42
- Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 16-17
- Imechapishwa: 09/02/2026
07 – Fadhilah za kumtaja Allaah
Tambua – ee msichana wa Uislamu – ya kwamba jambo bora zaidi mtu anaweza kujishughulisha wakati wake ni kumtaja Allaah, kumuomba, kumuomba msamaha na kusoma Qur-aan Tukufu. Hayo yanafanywa baada ya kutekeleza ´ibaadah za faradhi. Amesema (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا
“Enyi walioamini! Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru na msabihini asubuhi na jioni.”[1]
Imaam Ahmad amesimulia katika ”Musnad” yake ya kwamba kuna bwana mmoja ambaye alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Shari´ah za Kiislamu zimenilemea. Nieleze juu ya jambo ambalo nitajishughulisha nalo.” Akamjibu: ”Usiache ulimi wako kuwa na unyevunyevu kwa kumtaja Allaah.”
Ameipokea Imaam Ahmad, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah.
Miongoni mwa hayo ni Tasbiyh na Tahliyl. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kuna maneno mawili mepesi zaidi kwenye ulimi, mazito zaidi kwenye mizani na ni yenye kupendeza zaidi kwa Mwingi wa huruma:
سُبْحَانَ اللَّهِ ، وبِحَمْدِهِ سُبْحَانَ اللَّهِ الْعَظِيمِ
“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na sifa zote njema ni Zake. Allaah, hali ya kuwa ametukuka, ametakasika kutokamana na mapungufu.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ni manne:
سبحان الله، والحمد لله، ولا إله إلا الله، والله أكبر
”Allaah ametakasika na mapungufu, himdi zote njema anastahiki Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na Allaah ni Mkubwa.”
Haijalishi umeanza na yepi.”
Ameipokea Muslim.
[1] 33:41-42
Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 16-17
Imechapishwa: 09/02/2026
https://firqatunnajia.com/07-kumtaja-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket