07. Kukusanya kati ya swalah ya ijumaa na Dhuhr kwa wakati mmoja

Yale yanayotajwa kuhusu baadhi ya watu katika yale mambo yanayotokea katika baadhi ya miji ya Kiislamu nje ya nchi hii ambapo wanaswali Dhuhr pamoja na ijumaa hali ya kusema kwamba kunaposwaliwa swalah nyingi za ijumaa katika mji mmoja inaweza sio sahihi. Kwa hivyo inatupasa kuwa waangalifu na kufanya lililo salama zaidi kwa kuswali Dhuhr baada yake kwa kuchelea pengine imeswaliwa kwa njia ambayo haikuwekwa katika Shari´ah. Maoni haya ni kosa kabisa na ni Bid´ah. Ni kitendo kinachoenda kinyume na dalili za Shari´ah na yale waliyopita juu yake waislamu katika karne mbalimbali na katika katika miji mbalimbali mwanzoni mwa Umamah huu. Hakuhitajika kufanya ijumaa nyingi. Kwa hivyo haijuzu kuzua swalah ambayo haikuidhiniwa na Allaah (Subhaanah). Amewawajibishia waja kuswali swalah tano katika siku ya ijumaa na siku nyenginezo. Kwa hiyo haijuzu kuzusha swalah ya sita si katika siku ya ijumaa wala siku nyenginezo. Kwa sababu hayo yanakwenda kinyume na dalili za Shari´ah na yale waliyoafikiana Salaf wa Ummah huu. Allaah (Subhaanah) amesema:

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ

“Je, wanao washirika waliowaamuru dini yale ambayo Allaah hakuyatolea kwayo idhini?”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayezua katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”[2]

Muslim ameipokea kwa tamko lisemalo:

“Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu basi atarudishiwa mwenyewe.”[3]

Maana yake ni kwamba atarudishiwa mwenyewe.

[1] 42:21

[2] al-Bukhaariy (2499) na Muslim (3242).

[3] Muslim (3243).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 50-52
  • Imechapishwa: 01/12/2021