4 – Mitume Wake.
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanamini Mitume wote na kwamba Allaah ametuma Mitume. Mtume wa kwanza ni Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aadam (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) pia ni Mtume; ni Mtume kwa kizazi chake. Mtume wa mwisho ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mitume wote ni haki. Mitume wote wamefikisha Ujumbe wa Allaah. Mitume wote wametumwa kwa lengo la kuwalingania watu katika kumwabudu Allaah peke Yake na kumtii. Sambamba na hilo wanawatahadharisha shirki na maasi. Mitume wote hii ndio ilikuwa kazi yao kuanzia wa mwanzo wao Aadam mpaka wa mwisho wao Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameitwa kuwa ndiye Mtume wa kwanza kwa sababu yeye ndiye alikuwa Mtume wa kwanza aliyetumilizwa kwa waliokuwa katika ardhi baada ya kutokea shirki. Kabla ya hapo walikuwa katika Tawhiyd wakifuata Shari´ah ya Aadam (´alayhis-Swalaatu was-Salaam). Baada ya hapo ndipo kukatokea shirki katika watu wa Nuuh (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) kwa sababu ya kuvuka kwao mipaka kwa Wadd, Suwaa´, Yaghuuth, Ya´uuq na Nasr[1]. Hapo ndipo Allaah akawatumia Nuuh ili awalinganie katika kumuabudu Allaah peke Yake na kuwatahadharisha na adhabu ya Allaah. Pale walipoendelea na wakapuuza ndipo Allaah akawazamisha kwa mafuriko.
[1] Tazama “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy (4920).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 13-14
- Imechapishwa: 16/10/2024
4 – Mitume Wake.
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanamini Mitume wote na kwamba Allaah ametuma Mitume. Mtume wa kwanza ni Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aadam (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) pia ni Mtume; ni Mtume kwa kizazi chake. Mtume wa mwisho ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mitume wote ni haki. Mitume wote wamefikisha Ujumbe wa Allaah. Mitume wote wametumwa kwa lengo la kuwalingania watu katika kumwabudu Allaah peke Yake na kumtii. Sambamba na hilo wanawatahadharisha shirki na maasi. Mitume wote hii ndio ilikuwa kazi yao kuanzia wa mwanzo wao Aadam mpaka wa mwisho wao Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameitwa kuwa ndiye Mtume wa kwanza kwa sababu yeye ndiye alikuwa Mtume wa kwanza aliyetumilizwa kwa waliokuwa katika ardhi baada ya kutokea shirki. Kabla ya hapo walikuwa katika Tawhiyd wakifuata Shari´ah ya Aadam (´alayhis-Swalaatu was-Salaam). Baada ya hapo ndipo kukatokea shirki katika watu wa Nuuh (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) kwa sababu ya kuvuka kwao mipaka kwa Wadd, Suwaa´, Yaghuuth, Ya´uuq na Nasr[1]. Hapo ndipo Allaah akawatumia Nuuh ili awalinganie katika kumuabudu Allaah peke Yake na kuwatahadharisha na adhabu ya Allaah. Pale walipoendelea na wakapuuza ndipo Allaah akawazamisha kwa mafuriko.
[1] Tazama “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy (4920).
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 13-14
Imechapishwa: 16/10/2024
https://firqatunnajia.com/07-kuamini-mitume-kwa-njia-iliyoenea/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)