07. Je, bora kwa imamu ni yeye kubadilishabadilisha idadi ya zile Rak´ah za Tarawiyh?

Swali: Je, bora kwa imamu ni yeye kubadilishabadilisha idadi ya zile Rak´ah au bora ni kufupika na Rak´ah kumi na moja?

Jibu: Sitambui ubaya wa jambo hilo. Hapana neno iwapo baadhi ya nyusiku ataswali Rak´ah kumi na moja na nyusiku nyenginezo akaswali Rak´ah ishirini na tatu. Ni sawa pia endapo atazidisha. Wigo ni mpana inapokuja katika swalah ya usiku. Lakini ni vizuri akifupika na Rak´ah kumi na moja ili kuithibitisha Sunnah na ili watu waweze kutambua swalah yake wasije wakadhani kuwa amesahau.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 11
  • Imechapishwa: 10/04/2022