07. Imani inashuka na watu wanatofautiana katika imani

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amewagawa waumini katika mafungu matatu:

1- Mtu mwenye kuidhulumu nafsi yake. Ni mtenda dhambi mwenye imani pungufu.

2- Mtu aliye kati na kati.

3- Mtu anayeshindana juu ya matendo mema.

Amefanya mtenda dhambi kuwa chini ya mwema. Kuna ambao ni wema, wenye kushindana juu ya matendo mema na waliozidhulumu nafsi zao. Wale wenye kushindana juu ya matendo mema na walio kati na kati ndio wema na wale waliozidhulumu nafsi zao ni wale watenda maasi. Hili linafahamisha kuwa imani inashuka na watu wanatofautiana katika imani.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 09/10/2016