06. Tuhuma za Haddaadiyyah dhidi ya Ahl-us-Sunnah

Pamoja na hivyo Haddaadiyyah wanawatuhumu kuwa ni Murji-ah. Haddaadiyyah wanawapiga vita Ahl-us-Sunnah kwa uongo na uzushi. Murji-ah hawaonelei hivi. Wanaonelea madhambi hayaiathiri imani kitu kama ambavyo matendo mema hayaathiri kufuru. Wanaonelea kiumbe ambaye ni muovu kabisa ana imani kama ya Jibriyl na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunamuomba Allaah kinga dhidi ya Irjaa´ hii mbaya. Murji-ah al-Fuqahaa´ hawaonelei kuwa matendo yanaingia katika imani na hawaonelei kuwa inapanda na kushuka. Huu ni uhalifu mbaya sana wa Qur-aan ambayo inathibitisha kupanda kwa imani pamoja na Hadiyth zinazothibitisha kuwa imani inashuka. Bali kuna Aayah hata ambazo zinaashiria kuwa imani inashuka.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 17
  • Imechapishwa: 09/10/2016