07. Dalili ya kwamba kisa cha kusulubiwa msalabani ni cha uongo

Dalili ya kwanza: Injili inashuhudia ya kwamba ´Iysaa alikuwa anajulikana kati ya watu na alikuwa akihubiri kwenye msikiti wa Aqsa ambao walikuwa wakiuita hekalu ya Sulaymaan. Kwa ajili hiyo ndio maana hakukuwa haja yoyote kwa mayahudi kutoa vipande thelathini vya fedha kumpa mtu ili awaonyeshe naye:

“14Wakati huo mmoja kati ya wale kumi na mbili, jina lake Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani 15na akasema: “Mtanipa nini lau nitamsaliti kwenu?” Wakampimia vipande thelathini vya fedha. 16Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi muafaka ili apate kumsaliti.”[1]

“47Basi alipokuwa katika kusema Yuda akaja, mmoja wa wale kumi na mbili, na pamoja naye kundi kubwa wenye panga na marungu, wametumwa na wakuu wa makuhani na wazee wa watu. 48Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara: “Yule nitakayembusu, basi huyo ndiye, mkamateni.” 49Mara akamwendea Yesu, akamsalimia na kusema Rabi na kumbusu.”[2]

Dalili ya pili: Wanaeleza namna yule mwanafunzi wa wale kumi na mbili Yuda Iskariote alivyopata vipande thelathini vya fedha ili awaonyeshe ´Iysaa. Pindi walipomkamata akawarudishia pesa, akajuta, akajitenga mbali kutokamana na matendo yao na akajinyonga. Yote haya yalipitika ndani ya masaa ishirini na nne, jambo ambalo lina mgongano wa wazi kabisa.

Dalili ya tatu na ndio dalili kubwa inayotosha kufichua ubatilifu wa kisa hichi:

“11Naye Yesu akasimama mbele ya liwali; liwali akamuuliza: “Wewe ndiye mfalme wa mayahudi?” Yesu akamjibu: “Wewe ndiye umesema hivo.” 12Pindi aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee hakujibu kitu. 13Hapo ndipo Pilato akamwambia: “Husikii ni yepi wanayokushuhudia?” 14Hakujibu hata neno moja, hata liwali akastaajabu sana.”[3]

Kwa mujibu wa wakristo alinyamaza kwa sababu alikuwa anataka kusulubiwa ili aweze kufa kwa ajili ya ukombozi na madhambi ya watu. Hivyo basi, ni kwa nini alimuomba Allaah amsalimishe kutokamana na kikombe, yaani mauaji?

“39Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli na kuomba: “Baba yangu, ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke. Lakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.”[4]

Ni kwa nini alipiga kelele alipokuwa msalabani:

“46Karibu na saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema: “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” (Maana yake: Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?).”[5]

Ni vipi aliacha kubainisha ukweli ilihali alikuwa ni mfaswaha ambaye alikuwa akitoa hotuba kwa muda mrefu na akikaripia na akiwakemea wanawazuoni wa mayahudi? Mtu mwenye akili hawezi kuyasadikisha.

Ikiwa kisa cha msalaba na ukombozi ni batili, basi ukristo wote unabomoka kuanzia kwenye msingi.

[1] Matayo 26:14-16

[2] Matayo 26:47-49

[3] Matayo 27:11-14

[4] Matayo 26:39

[5] Matayo 27:46

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy al-Maghribiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Baraahiyn al-Injiylyyah ´alaa anna ´Iysaa daakhil fiyl-´Ubuudiyyah wa la hadhdhwa lahu fiyl-Uluuhiyyah, uk. 21-2
  • Imechapishwa: 16/10/2016