06. Dalili zaidi kwenye Injili ya kwamba ´Iysaa ni mwanadamu

“3Na huu ndio uzima wa milele: Wakutambue wewe, Mungu wa kweli wa pekee, na Yesu Kristo uliyemtuma.”[1]

“28Mmoja katika waandishi akaja na akawasikia wanavyojadili na kuona namna ambavyo Yesu amewajibu vyema na akafika na kumuuliza: “Katika maamrisho yote ni yapi yaliyo ya kwanza?” 29Yesu akamjibu: “Ya kwanza ni hii: Sikia, Israeli, Bwana, Mungu wetu ni Bwana mmoja, 30nawe unatakiwa kumpenda Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa uelewa wako wote na kwa nguvu zako zote.”[2]

“32Yule mwandishi akamwambia: “Hakika mwalimu, umesema kweli! Uliyosema: Mungu ni mmoja, hakuna mwingine isipokuwa yeye. 33Kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa uelewa wote na kwa nguvu zote na kumpenda jirani kama nafsi yako mwenyewe, ni zaidi kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhahibu zote pia.” 34Pindi Yesu alipoona kuwa amejibu kwa busara alimwambia: “Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu.” Tokea hapo hakuna yeyote aliyethubutu kumuuliza nena tena.”[3]

Masihi (´alayhis-Salaam) ameshuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, Mungu mmoja wa pekee, na kwamba yule mwenye kumuabudu Yeye peke yake ndiye ambaye yukaribu na ufalme Wake. Ina maana ya kwamba yule mwenye kumuabudu mwingine au akamgawa mara tatu yuko mbali kabisa na ufalme wa Allaah. Ambaye yumbali na ufalme wa Allaah basi huyo ni adui wa Allaah.

“32Siku hiyo na saa hiyo hakuna yeyote aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, isipokuwa Baba.”[4]

Mfano wa haya yametajwa katika Matayo ya Injili. Haya ndio yaliyotajwa katika Qur-aan, ya kwamba hakuna yeyote ajuaye Saa isipokuwa Allaah. Kwa hivyo unathibiti uanadamu wa kawaida wa ´Iysaa ilihali uungu unakuwa muhali na ukhurafi wa utatu unaangamia.

“16Yesu akamwambia: “Mariamu.” Akageuka na akamwambia: “Raboni!” (Ni kiebrania na maana yake ni mwalimu wangu). 17Yesu akamwambia: “Usiniguse, kwa maana bado sijapanda kwenda kwa Baba yangu. Nenda kwa ndugu zangu na uwaambie kuwa napanda kwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.”[5]

Hapa Masihi ameshuhudia ya kwamba Allaah ndiye Mungu wake na Mungu wao. Hakuna tofauti kati ya yeye na wao kutokana na kwamba wote ni wanadamu waja. Hivyo mwenye kusema ya kwamba Masihi ni mungu basi amemkadhibisha Masihi na amewakadhibisha Mitume na Manabii wote.

[1] Yohana 17:03

[2] Marko 12:28-30

[3] Marko 12:32-34

[4] Marko 13:32

[5] Yohana 20:16-17

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy al-Maghribiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Baraahiyn al-Injiylyyah ´alaa anna ´Iysaa daakhil fiyl-´Ubuudiyyah wa la hadhdhwa lahu fiyl-Uluuhiyyah, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 16/10/2016