7- Ahmad bin Hamdaan ash-Shaarikiy na Ahmad bin Sulaymaan al-Baswriy wametuhadithia: ar-Raffaa´ ametuhadithia: ´Umar bin Hafsw ametuhadithia: ´Aaswim bin ´Aliy al-Mas´uudiy ametuhadithia… ح Muhammad bin Mahmuud ametuhadithia: al-Idriysiy ametuhadithia: Abuu Sa´iyd az-Zaahid ametuhadithia: Ibn Karaabiyah ametuhadithia: ´Ubaydullaah ametuhadithia, kutoka kwa al-Mas´uudiy… ح Ametuhadithia kutoka kwa ´Amr bin Murrah, kutoka kwa Abuu ´Ubaydah, kutoka kwa Abuu Muusaa (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituhutubia mambo matano na kusema: “Allaah halali na wala haimstahikii Yeye kulala. Anaishusha mizani na kuinyanyua. Kwake kunapandishwa matendo ya usiku kabla ya mchana na matendo ya mchana kabla ya usiku. Pazia Yake ni Nuru; lau ataifunua, basi mwanga wa uso Wake ungeliunguza kila anachoona katika uumbaji Wake.”[1]

[1] Muslim (179).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 28
  • Imechapishwa: 12/01/2017