Amesema:

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ

“Nini kilichokuingizeni katika [Moto wa] Saqar?” Watasema: “Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali.”[1]

Amesema katika Aayah nyingine:

فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ

“Ole wao waswaliji.”[2]

Wanasema kuwa Allaah amewasema vibaya watu ambao hawaswali kwa kusema:

فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ

“Ole wao waswaliji.”

Halafu amesema juu ya watu walioingia Motoni kwa sababu hawakuwa katika waswaliji. Wakaitilia mashaka Qur-aan kwa sababu hiyo na wakadai kuwa ni yenye kujigonga.

Kuhusu maneno Yake:

فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ

“Ole wao waswaliji.”

wanaokusudiwa ni wanafiki:

الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ

”… ambao wanapuuza swalah zao.”[3]

Bi maana mpaka ukamalizika wakati wake:

الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ

”… ambao wanapuuza swalah zao.”[4]

Wanapoonekana, huswali, na wasipoonekana, haswali.

Kuhusu maneno Yake:

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ

“Nini kilichokuingizeni katika [Moto wa] Saqar?” Watasema: “Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali.”,

wanakusudiwa wapwekeshaji waumini. Hili wanatilia pia shaka mazanadiki[5].

[1] 74:42-43

[2] 107:4

[3] 107:6

[4] 107:6

[5] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com