06. Ulazima wa kuijua dini ya Uislamu kwa dalili

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kuijua dini ya Kiislamu kwa dalili

MAELEZO

Huu ni mlango mpana. Kwa sababu dini ya Uislamu chini yake ndio kuna ´ibaadah zote za kimaneno na kimatendo, zenye kuonekana na zilizojificha. Kunapotajwa “Uislamu” kumekusanya yale yote ambayo Allaah amewafaradhishia watu na ulimwengu wa majini katika mambo mbalimbali ya faradhi, mambo ya wajibu, makatazo na mengineyo katika mambo ya ´ibaadah ya Kishari´ah ambayo Allaah ameumba ulimwengu wa watu na ulimwengu wa majini kwa ajili yake. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ

”Hakika dini mbele ya Allaah ni Uislamu.”[1]

Amefupiza yale ambayo Ummah wanaamini ndani ya Uislamu. Kwa msemo mwingine ni yale mafunzo yote ya Uislamu yaliyokuja na mjumbe wa Uislamu.

Allaah (´Azza wa Jall) amekhabarisha kuwa anayetaka kumwabudu Allaah kwa dini isiyokuwa ya Uislamu kwamba ´ibaadah zake ni batili na maneno yake anarudishiwa mwenyewe. Amesema:

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

”Yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[2]

Wapotevu katika mayahudi, wakristo na wengineo wanaodai kwamba wako na Shari´h yao wamekhasirika. Ni lazima waachane na Shari´ah hiyo na ´ibaadah hizo wanazodai kuwa wameamrishwa kwazo katika Tawraat na Injiyl. Wanadai kuwa Qur-aan hii imeteremshwa kwa waarabu na kwamba inawahusu wao tu na si yenye kuwaenea viumbe wengine wa Allaah, madai ambayo ni batili. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameyabatilisha katika Aayah nyingi kwa kutaja ujumla na kuenea kwa ujumbe wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyabatilisha pale aliposema:

“Lau ndugu yangu Muusa angelikuwa hai basi isingelimuwezekani jengine isipokuwa kunifuata.”[3]

[1] 03:19

[2] 03:85

[3] Ahmad (03/338), at-Tirmidhiy (01/126) na kitabu ”as-Sunnah” (01/27) (50). Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy. Cheni ya wapokezi wake ni waaminifu isipokuwa Mujaalid ambaye ni Ibn Sa´iyd ni mdhaifu. Lakini hata hivyo Hadiyth ni nzuri. Ina njia zengine ambazo nimeziashiria katika “al-Mishkaah” (177) kasha nikataja baadhi yake katika “al-Irwaa´” (1589).

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Twariyqal-Usuwl ilaa idhwaah-ith-Thalaat-il-Usuwl, uk. 20-21
  • Imechapishwa: 18/11/2021