Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Wanasema nini kuhusu Hadiyth zinazozungumzia sifa ikiwa ni pamoja na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika nyoyo za waja ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa huruma.”[1]

MAELEZO

Aidha tunamthibitishia Allaah kuwa na vidole. Allaah Yeye mwenyewe amejithibitishia navyo. Tunathibitisha kuwa anaziendesha nyoyo za waja. Yeye (Subhaanah) anamwongoza Amtakaye na anampotosha Amtakaye. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika nyoyo za waja ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa huruma.”

hayana maana kuwa vidole vinagusana na moyo. Hakuna ulazima wa kimoja kipelekee katika kingine. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ

”… na mgeuko wa pepo na mawingu yanayotiishwa baina ya mbingu na ardhi… ”[2]

Kwa sababu tu upepo kuwepo kati ya mbingu na ardhi, haina maana kuwa vinagusana. Upepo uko kati ya mbingu na ardhi, lakini havikatamani na mbingu wala ardhi. Kitu kuwepo katikati hakilazimishi kukatamana na kugusana. Kwa hivyo tunaithibitisha Hadiyth kama ilivyokuja kwa njia inayolingana na utukufu na ukubwa wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kwa njia isiyopelekea kukamatana na kugusana.

[1] Muslim (2654), Ahmad (2/168) na an-Nasaa´iy (7739).

[2] 2:164

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 29
  • Imechapishwa: 24/07/2024