Aayah:

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“… kisha akalingana juu ya ´Arshi.”

inatakiwa kufahamika kihakika na kwamba maana yake ni kuwepo na kupanda juu ya ´Arshi. Hii ndio maana yake. Ama kuhusu kutawala, ni kitu hakikufupika juu ya ´Arshi, Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amekitawala kila kitu. Kwa maana nyingine ni kwamba anakimiliki na kukiendesha. Isitoshe Aayah isemayo:

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi.”[1]

 Kulingana juu kumetokea baada ya kuziumba mbingu na ardhi kwa siku sita. Inafahamisha mpangilio. Kwa mujibu wa ´Aqiydah ya watu hawa ni kwamba Allaah ameitawala ´Arshi baada ya kuishinda na hapo kabla ilikuwa inamilikiwa na wengine. Wakati mtawala anapoitawala nchi ni kuwa amewashinda maadui wake ndani ya nchi hiyo. Hii ni tafsiri batili. Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu cha kujitegemea akiraddi na kubatilisha tafsiri hii kwa njia ishirini.

[1] 07:54

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 28