06. Ni lazima kwa waumini kupupia swalah za mkusanyiko na ijumaa

Watu wengi hii leo wameshughulisha na mambo ya starehe na kutoka kwenda pikniki mpaka wameshughulishwa na swalah ya ijumaa. Matokeo yake wamenyimwa kusikiliza yale ambayo ndani yake kuna mawaidha na ukumbusho na ughafilikaji ukaendelea kwa kipindi kirefu. Mtu akiwa si mwenye kuhudhuria duara za elimu, hasikilizi Khutbah na wala hatilii umuhimu yale yanayonakiliwa kutoka kwa wanazuoni basi ughafilikaji wake unazidi. Pengine moyo wake ukawa mgumu mpaka akapigwa muhuri. Mwishowe anakuwa miongoni mwa waghafilikaji.

Ni lazima kwa muumini kupupia swalah ya ijumaa na swalah nyenginezo katika mkusanyiko ili afaidike na Khutbah, mihadhara na duara za elimu na ili wengine wapate kumuigiliza. Akiwa analazimika kufanya pikniki katika likizo, swalah ya ijumaa na siku ya alkhamisi, basi apupie awe karibu na mji. Ukifika wakati wa swalah basi aiendee na aswali ijumaa pamoja nao ili asikose ijumaa na asikose kheri hii tukufu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 50
  • Imechapishwa: 30/11/2021