06. Ni kweli kwamba haifai kwa wanachuoni kupigana radd?

Swali 06: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kusema kwamba leo haifai kwa wanachuoni kupigana radd wao kwa wao? Hoja yao ni kwamba kitendo hichi kinawafanya maadui kupata nguvu na kufarikisha umoja?

Jibu: Haya ni maneno ya batili na madai yasiyofaa. Makusudio ni kuharibu kitendo cha kuamrisha mema na kukataza maovu. Makusudio vilevile ni kuacha kubainisha haki. Asli ya aliyesema hivi ni Hasan al-Bannaa aliyesema:

“Waislamu wote, kuanzia dini yao, Qur-aan, yao, Mtume wao na Mtume wao ni mmoja. Kwa hivyo kusiletwe mpasuko.”

Kwa ajili hiyo ndio maana alikuwa akikusanya kati ya Salafiy na Suufiy, Shiy´iy na Mu´taziliy na huku akisema kwamba wote ni waislamu. Hili ni kutokana na kanuni aliyounda inayosema:

“Tunashirikiana katika yale tunayokubaliana na tunasameheana katika yale tunayotofautiana.”

Kanuni hii ni batili. Wanachuoni wameiraddi na kubainisha makosa ilionayo.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 16/07/2017