06. Kumuomba Allaah wakati wa Allaah aihifadhi nafsi ikirudi, na airehemu ikifishwa

62 – ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) alimwamrisha bwana mmoja anapotaka kulala aseme:

اللّهُـمَّ إِنَّـكَ خَلَـقْتَ نَفْسـي وَأَنْـتَ تَوَفّـاهـا لَكَ ممَـاتـها وَمَحْـياها، إِنْ أَحْيَيْـتَها فاحْفَظْـها، وَإِنْ أَمَتَّـها فَاغْفِـرْ لَـها. اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ العـافِـيَة

”Ee Allaah! Hakika Wewe ndiye umeiumba nafsi yangu na Wewe ndiye utaifisha. Ni Kwako kufa na kuhuika kwake. Ukiipa uhai, basi ihifadhi, na ukiifisha, basi isamehe. Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba hifadhi na salama.”[9]

Bwana mmoja akamuuliza: “Je, umeyasikia haya kutoka kwa ´Umar?” Akasema: “Kutoka kwa mbora kuliko ´Umar; kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Katika Dhikr hii kuna kutambua ya kwamba Allaah (Ta´ala) ndiye Muumbaji Mwenye kufisha. Yeye ndiye Allaah anayesifiwa kuumba, kuhuisha na kufisha. Ndani yake kuna kumuomba Allaah aihifadhi nafsi hii inaporudi duniani au aisamehe ikiwa Allaah ataichukua. Ndani yake pia kuna kumuomba Allaah usalama katika hali zote mbili.

[1] Muslim (2712).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 70
  • Imechapishwa: 21/10/2025