59 – Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:
“Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapotaka kulala husema:
بِاسْـمِكَ اللّهُـمَّ أَمـوتُ وَأَحْـيا
”Kwa jina lako, ee Allaah, ninakufa na ninakuwa hai.”
Na anapoamka kutoka usingizini husema:
الْحَمْدُ للَّهِ الَّذِي أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا، وَإِلَيْهِ النُّشُورُ
“Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye ametupa uhai baada ya kutufisha na Kwake ndiko tutafufuliwa.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy.
60 – al-Baraa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapotaka kulala:
اللهُمَّ بِاسْمِكَ أحْيَا وَبِاسْمِكَ أُمُوتُ
“Ee Allaah, kwa jina Lako nakuwa hai na kwa jina Lako ninakufa.”
Na anapoamka husema:

“Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye ametupa uhai baada ya kutufisha na Kwake ndiko tutafufuliwa.”[2]
Ameipokea Muslim.
61 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kupitia kwake ya kwamba alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapoenda kitandani mwake husema:
الـحَمْدُ للهِ الَّذي أَطْـعَمَنا وَسَقـانا، وَكَفـانا، وَآوانا، فَكَـمْ مِمَّـنْ لا كـافِيَ لَـهُ وَلا مُؤْوِيَ
”Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, ambaye ametulisha, akatunywesha, akatutosheleza na akatuhifadhi. Kwani ni wangapi ambao hawana wa kuwatosheleza wala wa kuwahifadhi!”[3]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Ni watu wengi wasiokuwa na mwenye kuwatosheleza wala mwenye kuwahifadhi katika ardhi ya Allaah iliyo pana. Hadiyth hii inafahamisha kuwa Dhikr hii inapendeza, kukumbuka neema za Allaah (´Azza wa Jall) na kumsifu wakati wa kulala.
[1] al-Bukhaariy (6324).
[2] al-Bukhaariy (6312) na Muslim (2711).
[3] Muslim (2715).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 68
- Imechapishwa: 21/10/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 68
Imechapishwa: 21/10/2025
https://firqatunnajia.com/05-dhikr-ya-kumsifu-allaah-na-kukumbuka-neema-zake-wakati-wa-kulala/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket