63 – Suhayl amesema: “Abu Swaalih alikuwa akituamrisha pindi anapotaka mmoja wetu kulala alalie ubavu wake wa kulia, kisha aseme:
اللّهُـمَّ رَبَّ السّمـواتِ وَرَبَّ العَـرْشِ العَظـيم، رَبَّنـا وَرَبَّ كُـلِّ شَـيءٍ، فالِـقَ الحَـبِّ وَالنَّـوى، وَمُـنَزِّلَ التَّـوْراةِ وَالإنْجـيلِ والفُـرْقانِ. أَعُـوذُ بِـكَ مِن شَـرِّ كُـلِّ شَـيءٍ أَنْـتَ آخِـذٌ بِنـاصِـيَتِهِ. اللّهُـمَّ أَنْـتَ الأوَّلُ فَلَـيسَ قَبْـلَكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الآخِـرُ فَلَـيسَ بَعْـدَكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الظّـاهِـرُ فَلَـيْسَ فَـوْقَـكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الْبـاطِـنُ فَلَـيْسَ دونَـكَ شَيءٌ، اقـْضِ عَنّـا الـدَّيْـنَ وَأَغْـنِنـا مِنَ الفَـقْرِ
”Ee Allaah, Mola wa mbingu na Mola wa ’Arshi tukufu. Mola wetu na Mola wa kila kitu. Mpasuaji wa mbegu na kokwa na aliyeteremsha Tawraat, Injiyl na Qur-aan. Najilinda Kwako kutokamana na shari ya kila kitu; Wewe ndiye Mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah! Wewe ndiye wa Mwanzo, hakuna kitu chochote kabla Yako. Wewe ndiye wa Mwisho, hakuna kitu chochote baada Yako. Wewe ndiye Uliye juu, hakuna kitu chochote juu Yako. Wewe ndiye Uliye karibu, hakuna kitu chochote kilichofichikana Kwako. Tulipie madeni yetu na utuepushe na ufakiri.”[1]
Hayo yalikuwa yakisimuliwa pia kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Najilinda Kwako kutokamana na shari ya kila kitu… ”
Bi maana kutokana shari ya kila kitu katika viumbe, kwa sababu kila kitu kiko ndani ya ufalme Wake na Yeye ndiye Mwenye kushika utosi Wake. Ni kana kwamba amejilinda kutokana na shari zote.

“Tulipie madeni yetu… “
Mtu anatakiwa kuomba du´aa hii ingawa hana deni lolote. Mtu anaweza kusema kuwa madeni imekusanya deni la Allaah na madeni ya waja.

“… na utuepushe na ufakiri.”
Ufakiri pia ni wenye kuenea na umekusanya ufakiri wa nafsi na uchache wa kile kilichoko mkononi. Kila mtu aombe du´aa hii. Ni mwenye kumuhitaji Allaah kwa ajili ya kumbakiza yeye na kumbakizia kile alichonacho.
Ndani yake kuna kufanya Tawassul kwa Allaah kutokana na matendo Yake, uumbaji Wake na kupasua Kwake mbegu na kokwa, kuteremsha Kwake Vitabu, majina na sifa Zake.
[1] Muslim (2713).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 71
- Imechapishwa: 21/10/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 71
Imechapishwa: 21/10/2025
https://firqatunnajia.com/07-dhikr-kuhusu-allaah-kukulinda-na-shari-ya-kila-kiumbe-kukulipia-madeni-na-tawassul/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket