06. Hadiyth “Yule mwenye kutema makohozi upande wa Qiblah atafufuliwa siku ya Qiyaamah… “

285 – Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

يُبعثُ صاحب النخامة في القبلة يوم القيامة وهى في وجهه

“Yule mwenye kutema makohozi upande wa Qiblah atafufuliwa siku ya Qiyaamah na akiwa nayo usoni mwake[1].”[2]

Ameipokea al-Bazzaar, Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake, na hili ni tamko lake, na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Alama ya unyonge, dharau na kufanya uzembe mbele ya Mola wake akiwa anaswali kwenye Nyumba ya Mola Wake.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/235)
  • Imechapishwa: 15/11/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy