06. Hadiyth “Walikuwa wakikata kila kitu ambacho kimepatwa na mkojo… “

162 – ´Abdur-Rahmaan bin Hasanah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitujia na mkononi mwake akiwa na ngao ya ngozi. Akaiweka chini, kisha akaketi chini na kuanza kukojoa kuielekea[1]. Mtu mmoja akasema: “Mtazameni, anakojoa kama anavokojoa mwanamke.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamsikia  na akasema: “Ole wako! Hukujua yaliyowafika wana wa israaiyl? Walikuwa wakikata kila kitu ambacho kimepatwa na mkojo. Kwa vile alikuwa amewakataza akaadhibiwa ndani ya kaburi lake.”[2]

Ameipokea Ibn Maajah na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Alikuwa anaiweka imzuie kutokamana na watu wasimuone.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/178)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy