06. Hadiyth “Msiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja au mbili… “

Haafidhw ´Abdul-Ghaniy al-Maqdisiy al-Hanbaliy (Rahimahu Allaah) ameema:

185 – ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Mkiuona fungeni na mkiuona fungueni. Mkifunikwa na mawingu basi ikadirieni.”[1]

MAELEZO

Hadiyth hii inaeleza kuwa watu wanafunga Ramadhaan kwa kuona mwezi mwandamo. Hadiyth nyingine inasema:

“Mkiona basi fungeni, na mkiona basi fungulieni. Ikiwa imefichika kwenu basi kamilisheni siku thelathini.”[2]

Imekuja katika tamko jengine:

“Fungeni kwa kuonekana kwake na fungueni kwa kuonekana kwake. Ikiwa imefichika kwenu basi kamilisheni hesabu ya Sha’baan kuwa siku thelathini.”[3]

Kwa maana ya kwamba kamilisheni mwezi wa Sha’baan siku thelathini ikiwa mwezi mwandamo haukuonekana kutokana na mawingu au wingu zito.

[1] al-Bukhaariy (1900) na Muslim (1080).

[2] Muslim (1081).

[3] al-Bukhaariy (1909).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr Dhil-In´am bisharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/436)
  • Imechapishwa: 16/02/2025