222 – Abu Rawh al-Kulaa amesema:

صلّى بنا نبيُّ الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – صلاةً فقرأ فيها بسورةِ (الروم) ، فلُبِّس عليه بعضُها، فقال: إنما لَبِّسَ علينا الشيطانُ القراءةَ من أجلِ أقوامٍ يأتون الصلاةَ بغيرِ وضوءٍ، فإذا أتيتم الصلاةَ، فأحسنوا الوضوءَ

“Siku moja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituswalisha na akasoma Suurah “ar-Ruum”, akatatizwa na baadhi ya Aayah ambapo akasema: “Hakika aliyetutazika katika kisomo ni shaytwaan kwa sababu ya watu wanaokuja kuswali pasi na wudhuu´. Kwa hivyo, mnapokuja kuswali basi tawadheni vizuri.”[1]

Imekuja katika upokezi mwingine:

فتردَّدَ في آيةٍ، فلما انصرفَ قال: إنه لُبِّسَ علينا القرآنُ؛ أنّ أقواماً منكم يصلُّون معنا لا يُحسنون الوضوءَ، فَمَنْ شهدَ الصلاةَ معنا فليُحْسِن الوضوء

“Akasitasita katika Aayah. Alipomaliza akasema: “Tumetatizwa Qur-aan kwa sababu kuna watu katika nyinyi wanaoswali nasi wasiotawadha vizuri. Yule anayeswali pamoja nasi basi atawadhe vizuri.”

Ameipokea namna hii Ahmad.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/207)
  • Imechapishwa: 21/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy