5- Misiba inayompata muislamu katika afya yake, familia yake, mtoto wake, mali yake, biashara yake na mfano wa hayo basi anatakiwa kuyakabili kwa kusubiri na kutarajia malipo kutoka kwa Allaah. Muislamu kama huyo ananyanyuliwa daraja mbele ya Allaah (´Azza wa Jall). Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ
“Bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao [katika kazi zenu]. Wabashirie wale wenye kusubiri ambao unapowafika msiba basi husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea – hao zitakuwa juu yao baraka kutoka kwa Mola wao na rehema na hao ndio wenye kuongoka.”[1]
Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) anampa majaribio mja Wake ili aweze kusikia kulalamika kwake, kunyenyekea kwake, kuomba kwake, kusubiri kwake na kuridhia kwake yale ambayo Allaah amempangia. Allaah (Subhaanah) anaona mitihani anayowapa waja Wake, anaona na kujua kila kitu ambapo anamlipa kila mmoja kutegemea na nia yake. Kwa ajili hiyo yule mwenye kujaribiwa kitu katika mtihani wowote basi ni juu yake kutaraji malipo kutoka kwa Allaah na ayapokee kwa kuwa na subira na kuridhia ili afuzu thawabu za wenye kusubiri sambamba na hilo yule aliyesalimishwa anatakiwa kumshukuru Allaah ili afuzu thawabu za wale wenye kushukuru.
[1] 02:155-157
- Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://ar.islamway.net/article/80439/%D9%81%D9%8A%D8%B1%D9%88%D8%B3-%D9%83%D9%88%D8%B1%D9%88%D9%86%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D8%AF%D9%8A%D8%AF-%D9%81%D9%8A%D8%B1%D9%88%D8%B3-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%8A%D9%86
- Imechapishwa: 12/03/2020
5- Misiba inayompata muislamu katika afya yake, familia yake, mtoto wake, mali yake, biashara yake na mfano wa hayo basi anatakiwa kuyakabili kwa kusubiri na kutarajia malipo kutoka kwa Allaah. Muislamu kama huyo ananyanyuliwa daraja mbele ya Allaah (´Azza wa Jall). Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ
“Bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao [katika kazi zenu]. Wabashirie wale wenye kusubiri ambao unapowafika msiba basi husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea – hao zitakuwa juu yao baraka kutoka kwa Mola wao na rehema na hao ndio wenye kuongoka.”[1]
Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) anampa majaribio mja Wake ili aweze kusikia kulalamika kwake, kunyenyekea kwake, kuomba kwake, kusubiri kwake na kuridhia kwake yale ambayo Allaah amempangia. Allaah (Subhaanah) anaona mitihani anayowapa waja Wake, anaona na kujua kila kitu ambapo anamlipa kila mmoja kutegemea na nia yake. Kwa ajili hiyo yule mwenye kujaribiwa kitu katika mtihani wowote basi ni juu yake kutaraji malipo kutoka kwa Allaah na ayapokee kwa kuwa na subira na kuridhia ili afuzu thawabu za wenye kusubiri sambamba na hilo yule aliyesalimishwa anatakiwa kumshukuru Allaah ili afuzu thawabu za wale wenye kushukuru.
[1] 02:155-157
Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://ar.islamway.net/article/80439/%D9%81%D9%8A%D8%B1%D9%88%D8%B3-%D9%83%D9%88%D8%B1%D9%88%D9%86%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D8%AF%D9%8A%D8%AF-%D9%81%D9%8A%D8%B1%D9%88%D8%B3-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%8A%D9%86
Imechapishwa: 12/03/2020
https://firqatunnajia.com/05-virusi-vya-corona-kuwa-na-subira-na-mshukuru-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)