Swali: Je, kumepokelewa pongezi kwa kuingia mwezi wa Ramadhaan? Nimwambie nini akinipongeza mtu?

Jibu: Imepokelewa kwamba Salaf walikuwa wakipeana pongezi kwa kuingia mwezi wa Ramadhaan. Hakuna neno katika hili. Kwa mfano anaweza kusema “mwezi uliobarikiwa” (شهر مبارك), “Allaah akubarikie mwezi wako” (بارك الله لك في شهرك) au mfano wa hayo. Yule mwenye kupongezwa ajibu mfano wa vile alivyopongezwa. Anaweza kwa mfano kujibu “nawe upate mfano wa hivo” (ولك بمثل هذا), “Uwe ni wenye baraka kwako pia” (وهو مبارك عليه) au yale yatayomfurahisha yule mwenye kupongeza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1576
  • Imechapishwa: 12/03/2020