4- Sifa ya nne: Mashaytwaan wale waasi wanafungwa minyororo[1] na wanashindwa kuyafanya yale waliokuwa wanaweza kuwafanyia waja wa Allaah wema katika kuwapotosha kutokamana na haki na kuwazuia kutokamana na kheri. Hii ni njia moja wapo ya Allaah kuwasaidia kwa kuwazuilia adui yao ambaye analingania kundi lake ili wawe miongoni mwa watu wa Motoni. Kwa ajili hiyo ndio maana utaona waja wema wana shauku katika mambo ya kheri na kujiepusha na shari katika mwezi huu zaidi kuliko wakati mwingine.

[1] al-Bukhaariy na na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 10
  • Imechapishwa: 02/04/2020