Shahaadah haimnufaishi kitu mwenye nayo isipokuwa kwa kutimia sharti saba:
1 – Utambuzi wa kile kilichokanushwa na kuthibitishwa. Anayeitamka pasi na kujua maana yake na yale inayopelekea, basi haitomfaa kitu. Kwa kuwa hakuitakidi yale inayofahamisha. Ni kama mfano wa ambaye anazungumza lugha asiyoifahamu.
2 – Yakini ambayo ni kuwa na utambuzi kamilifu wa makanusho haya pasi na kuwa na mashaka yoyote.
3 – Kumtakasia nia Allaah pekee ambayo ni kinyume chake ni shirki. Haya ndio yanayofahamishwa na shahaadah.
4 – Ukweli ambao kinyume chake ni unafiki. Wanaitamka kwa ndimi zao pasi na kuamini yale yanayofahamishwa nayo.
5 – Kulipenda neno hili na maana yake na pia kuyafurahikia tofauti na wanavyofanya wanafiki.
6 – Kunyenyekea kwa kulitekelezea haki zake. Haki zake ni yale matendo ya wajibu hali ya kumtakasia nia Allaah na kutafuta radhi Zake. Haya ndio yanayopelekea kwayo.
7 – Kuikubali ambako kinyume chake ni kurudisha. Hilo linahakikishwa kwa kunyenyekea yale maamrisho ya Allaah na kuacha makatazo Yake.
Sharti hizi zimefikiwa na wanazuoni kutoka katika dalili za Qur-aan na Sunnah ambayo yamekuja kulizungumzia neno hili tukufu na kubainisha haki zake, kanuni zake na kwamba sio mtamshi yanayotamkwa tu kwa ulimi.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ma´naa laa ilaaha illa Allaah, uk. 18-19
- Imechapishwa: 23/09/2023
Shahaadah haimnufaishi kitu mwenye nayo isipokuwa kwa kutimia sharti saba:
1 – Utambuzi wa kile kilichokanushwa na kuthibitishwa. Anayeitamka pasi na kujua maana yake na yale inayopelekea, basi haitomfaa kitu. Kwa kuwa hakuitakidi yale inayofahamisha. Ni kama mfano wa ambaye anazungumza lugha asiyoifahamu.
2 – Yakini ambayo ni kuwa na utambuzi kamilifu wa makanusho haya pasi na kuwa na mashaka yoyote.
3 – Kumtakasia nia Allaah pekee ambayo ni kinyume chake ni shirki. Haya ndio yanayofahamishwa na shahaadah.
4 – Ukweli ambao kinyume chake ni unafiki. Wanaitamka kwa ndimi zao pasi na kuamini yale yanayofahamishwa nayo.
5 – Kulipenda neno hili na maana yake na pia kuyafurahikia tofauti na wanavyofanya wanafiki.
6 – Kunyenyekea kwa kulitekelezea haki zake. Haki zake ni yale matendo ya wajibu hali ya kumtakasia nia Allaah na kutafuta radhi Zake. Haya ndio yanayopelekea kwayo.
7 – Kuikubali ambako kinyume chake ni kurudisha. Hilo linahakikishwa kwa kunyenyekea yale maamrisho ya Allaah na kuacha makatazo Yake.
Sharti hizi zimefikiwa na wanazuoni kutoka katika dalili za Qur-aan na Sunnah ambayo yamekuja kulizungumzia neno hili tukufu na kubainisha haki zake, kanuni zake na kwamba sio mtamshi yanayotamkwa tu kwa ulimi.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ma´naa laa ilaaha illa Allaah, uk. 18-19
Imechapishwa: 23/09/2023
https://firqatunnajia.com/05-sharti-za-shahaadah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)