Anas ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu siku ya ijumaa:

“Hiyo ndio siku ambayo Mola wenu amelingana juu ya juu ya ´Arshi.”[1]

Ameipokea ash-Shaafi´iy.

Ibn ´Abbaas ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ ، وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ ، يُحْيِي وَيُمِيتُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Hapana mwabudiwa isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana na mshirika. Ufalme Wake na himdi Zake. Anahuisha na kufisha Naye juu ya kila kitu ni Muweza.”

isipokuwa mbingu hupasuka mpaka maneno hayo yamfikie Allaah (´Azza wa Jall).”

Ameipokea Abu Ahmad al-´Assaal.

Abu Ja´far ar-Raaziy amesimulia kutoka kwa ´Aasim, kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume wa  Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Alipotupwa Ibraahiym (´alayhis-Salaam) ndani ya moto alisema: ”Ee Mola wangu! Hakika Wewe ni wa Mmoja juu ya mbingu nami ni wa pekee ardhini ninayekuabudu.”[2]

Hadiyth ni nzuri.

Abud-Dardaa´ amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote kati yenu anayehisi maumivu basi na aseme:

رَبَّنَا اللَّهُ الَّذِي فِي السَّمَاءِ تَقَدَّسَ اسْمُكَ ، أَمْرُكَ فِي السَّمَاءِ وَالأَرْضِ كَمَا رَحْمَتُكَ فِي السَّمَاءِ ، اغْفِرْ لَنَا حُوبَنَا وَخَطَايَانَا أَنْتَ رَبُّ الطَّيِّبِينَ ، أَنْزِلْ رَحْمَةً مِنْ رَحْمَتِكَ وَشِفَاءً مِنْ شِفَائِكَ عَلَى هَذَا الْوَجَعِ

“Mola wetu ni Allaah ambaye yuko juu ya mbingu. Limetakasika jina Lako. Amri Yako iko mbinguni na ardhini kama ambavyo huruma Yako iko mbinguni. Tusamehe madhambi na makosa yetu. Wewe ni Mola wa wazuri. Teremsha rehema miongoni mwa rehema Zako na dawa miongoni mwa dawa Zako kwa huyu anayehisi maumivu.”

Hivyo atapona.”[3]

Ameipokea Abu Daawuud na wengineo.

´Imraan bin Khaalid bin Twaliyq bin Muhammad bin ´Imraan bin Huswayn amesema: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kwamba:

”Quraysh walikuja kwa al-Huswayn, ambaye walikuwa wakimuheshimu, na wakasema: “Zungumza na bwana huyu, kwani anazungumzia vibaya miungu yetu na anawatukana.” Basi wakaja naye hadi wakakaa karibu na mlango wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakaketi chini na yeye al-Huswayn akaingia ndani. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomwona akasema: “Mfanyieni nafasi mzee.”  Wakafanya hivo. ´Imraan na Maswahabah walikuwa wengi. al-Huswayn akasema: “Ni nini hiki tunachosikia juu yako kwamba unawatukana miungu yetu ilihali baba yako alikuwa mtu mtukufu?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee al-Huswayn, hakika baba yangu na baba yako wote wawili wako Motoni. Ee al-Huswayn, ni miungu mingapi unaiabudu hii leo?” Akasema: “Saba ardhini na mungu mmoja juu mbinguni.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuuliza: “Basi ikikupata dhara, unamwomba nani?” Akasema: “Aliyeko juu mbinguni.” Akasema: “Na mali ikiharibika, unamwomba nani?” Akasema: “Aliyeko juu mbinguni.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Basi anakujibu Yeye peke Yake na bado unawashirikisha wengine pamoja Naye?”[4]

Ameipokea imamu wa maimaam Abu Bakr Muhammad bin Ishaaq bin Khuzaymah katika ”Kitaab-ut-Tawhiyd” kupitia kwa Rajaa´ bin Muhammad, kutoka kwa ´Imraan bin Khaalid. Amesema kuwa ”ameitaja katika ”Kitaab-ud-Du´aa´.”

[1] ash-Shaafi´iy katika ”al-Musnad” (374). adh-Dhahabiy amesema kuwa ”Ibraahiym na Muusa ni wanyonge” (al-´Uluww, uk. 30).

[2] Nzuri kwa mujibu wa adh-Dhahabiy katika “al-´Uluww”, uk. 2, na “Kitaab-ul-´Arsh” (50).

[3] Abu Daawuud (3892), an-Nasaa’iy (10877) na al-Haakim (1/344). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (3892).

[4] Ibn Khuzaymah katika ”Kitaab-ut-Tawhiyd”, uk. 120, ambaye ameisahihisha, al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat”, uk. 534, na adh-Dhahabiy katika ”al-´Uluww, uk. 24, ambaye amesema kuwa ”´Imraan ni dhaifu”.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 34-37
  • Imechapishwa: 21/12/2025