05. Radd kwa yule mwenye kuonelea kuwa Hadiyth kuhusu sifa za Allaah zinatakiwa kutosambazwa

5- ´Abdul-Jabbaar bin Muhammad as-Siraajiy ametuhadithia: Muhammad bin Ahmad bin Mahbuub ametuhadithia: Abuu ´Iysaa at-Tirmidhiy ametuhadithia: ´Abdul-Wahhaab al-Baghdaadiy al-Warraaq ametuhadithia: Mu´aadh bin Mu´aadh ametuhadithia, kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Thaabit al-Bunaaniy, kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusiana na manneo Yake (´Azza wa Jall):

فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا

“Pindi Mola wako alipojionyesha kwenye mlima, akaufanya uvurugike kuwa vumbi.” (07:143)

Anas (Radhiya Allaah ´anh) akaashiria ncha ya kidole chake kidogo, Thaabit al-Bunaaniy akafanya hali kadhalika. Ndipo Humayd at-Twawiyl akasema: “Unakusudia nini, ee Abuu Muhammad?” Ndipo Thaabit akanyanyua mkono wake na akampiga kifua chake kwa nguvu kabisa. Halafu akamwambia: “Wewe ni nani, ee Humayd? Wewe uko wapi, ee Humayd? Anas bin Maalik amenieleza haya kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wewe unasema: “Unamaanisha nini kwa haya?”?”[1]

[1] Ahmad (3/125), at-Tirmidhiy (3074) aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri, geni na Swahiyh, Ibn Khuzaymah, uk. 74, na al-Haakim (2/320) aliyesema kuwa Hadiyth ni Swahiyh kwa mujibu wa masharti ya Muslim. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (480-485).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 26
  • Imechapishwa: 09/01/2017