05. Ni lazima kutaja mazuri ya mtu wakati wa kumraddi?

Swali 05: Je, ni katika mfumo wa Salaf kutaja mazuri na mabaya ya mtu wakati wa kutoa nasaha?

Jibu: Jambo hili sio katika mfumo wa Salaf. Hakuna yeyote aliyesema hivi isipokuwa katika wakati wa leo. Haya yamesemwa na al-Ikhwaan al-Muslimuun na wafuasi wao. Wanasema kuwa ni lazima kupima baina ya mazuri na mabaya. Hili ni batili na halina msingi katika haki, Qur-aan na Sunnah. Hakuna yeyote katika Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala katika Salaf aliyesema hivo.

Wakati Faatwimah bint Qays alipomtaka ushauri Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kuolewa na Mu´aawiyah au Abu Jahm akamwambia:

“Kuhusu Mu´aawiyah hana pesa kabisa na Abu Jahm ni mwenye kuwapiga wanawake.”[1]

Hakutaja chochote katika mazuri yao.

Endapo tutataka kuona dalili hizi, basi tutazipata kwenye kitabu alichokusanya muheshimiwa Shaykh Salafiy Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy (Hafidhwahu Allaah) ambapo amewaraddi wale wenye kuzungumza kwa mfumo huu.

[1] Muslim (1480).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 16/07/2017