04. Kuna Salafiyyah ya kale na ya sasa?

Swali 04: Je, kuna Salafiyyah ya zamani na Salafiyyah mpya au kuna Salafiyyah moja peke yake?

Jibu: Salafiyyah ni moja peke yake. Anayedai kuwa kuna Salafiyyah ya zamani na Salafiyayh mpya amesema uongo.

Lau tutatazama juu ya ´Aqiydah ya Salaf, kuanzia wakati wa Maswahabah mpaka hii leo, basi tutaona kuwa ´Aqiydah ni moja. Haitofautiani kamwe, hata kama watatofautiana katika mambo madogo madogo ambayo hayahusiani na misingi. Wanatofautiana katika mambo madogo madogo. Pamoja na hivyo hawaashiriani vidole kwa hayo. Hii ndio njia ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Ama inapokuja katika ´Aqiydah, mfumo wao ni mmoja tangu wakati wa Maswahabah mpaka hii leo.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 16/07/2017