1- Mwenye busara anatakiwa kutambua kuwa akili ina matawi ya maamrisho na makatazo ambayo analazimika kuyatambua na kuitumia katika wakati muafaka ili kujitofautisha na ambaye si msomi.

2- Tawi la kwanza la akili ni kumcha Allaah na kuirekebisha nyoyo. Mwenye kurekebisha undani wake, basi Allaah atarekebisha uinje wake. Mwenye kuharibu undani wake, basi Allaah atauharibu uinje wake.

3- Maalik bin Diynaar amesema:

“Fanya biashara na Allaah basi utapata faida bila ya bidhaa yoyote.”

4- Nguzo ya utiifu duniani inapatikana katika kurekebisha undani wake na kuyaepuka yenye kuuharibu.

5- Ni wajibu kwa mwenye busara kutilia umuhimu undani wake na kuuchunga moyo wake katika hali zote. Moyo hauharibiwa isipokuwa pale ambapo wakati unachafuliwa na starehe inaharibiwa.

6- Maalik bin Diynaar amesema:

“Moyo usiokuwa na huzuni huharibika kama nyumba isiyokuwa na wakazi. Nyoyo za wema zinaiva kwa matendo mema. Nyoyo za waovu zinawiva kwa madhambi. Allaah anayaona yale mnayofikiria. Hivyo basi tazameni yale mnayofikiria – Allaah akurehemu.”

7- al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Nyinyi mmesimama hapa na mnasubiri wakati wenu ukijieni. Mtapokufa mtakutana na khabari. Hivyo chukueni kutoka kwa yale mlionayo kwa ajili ya kile chenye kuwasubiri.”

8- Ni wajibu kwa mwenye akili kuchukua kutoka kwa yale alionayo katika uchaji Allaah na matendo mema kwa yale yanayomsubiri kwa kurekebisha undani wake na kutupilia mbali yale yote yanayoharibu utiifu.

9- Khaalid ar-Rab´iy amesema:

“Luqmaan alikuwa ni mtumwa wa kihabeshi na serelama. Siku moja bosi waka akamuamrisha amchinje kondoo na akamwambia: “Nipe viungo viwili bora kabisa vya kondoo.” Luqmaan akamletea ulimi na moyo. Baada ya siku mbili bosi wake akamuamrisha achinje tena kondoo na kumwambia: “Nipe viungo viwili vibaya kabisa vya kondoo.” Luqmaan akampa ulimi na moyo. Hapo ndipo bosi wake akasema: “Nilipokwambia ulete viungo viwili bora kabisa uliniletea ulimi na moyo na pindi nilikwambia uniletee viungo viwili vibaya kabisa uliniletea ulimi na moyo.” Luqmaan akasema: “Viwili hivyo vikiwa vizuri vinakuwa bora kabisa na vikiwa vibaya vinakuwa vibaya kabisa.”

Swaalih bin Hassaan amesema:

“Niliingia kwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz na nikamsikia akisema: “Mja hamchi Allaah mpaka aonje ladha ya udhalilifu.”

10- Mwenye busara anaungalia moyo wake katika kipindi cha maisha, anaitenga mbali nafsi yake kutokamana na makatazo yote, anafanya aina mbalimbali ya yale yaliyoamrishwa na anakuwa makini pindi anapochoshwa. Hata hivyo mtu hatohakikisha yote tuliyoyataja mpaka kikweli ajihakikishe juu ta matendo yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 26-29
  • Imechapishwa: 12/11/2016