1- Shu´bah amesema:

“Akili zetu ni ndogo. Tunapotangamana na watu wenye akili ndogo kuliko, basi kidogo hicho kinapotea. Ninapomuona mtu anatangamana na ambaye ana akili ndogo kuliko, basi huanza kumchukia vibaya.”

2- Kitu na sifa ya kwanza ambayo mtu anaweza kupata hapa duniani ni akili. Ndio kitu bora ambacho Allaah anaweza kuwapa waja Wake. Kwa hivyo haifai kuchafua neema ya Allaah kwa kukaa na mtu ambaye yuko kinyume kabisa.

3- Ni wajibu kwa mwenye busara atangamane kwa uzuri na anyamaze kwa muda mrefu. Hilo ni katika tabia za Mitume. Kama ambavyo vilevile kutangamana kwa ubaya na kutoacha kuzungumza ni katika tabia ya wala khasara.

4- Aliye na busara haweki matumaini mengi. Mwenye kuweka matumaini mengi matendo yake hudhoofika. Anayekufa matumaini yake hayatomfaa kitu.

5- Mwenye busara hapambani pasi na silaha. Hajadili pasi na hoja. Havutani pasi na nguvu. Akili inazihuisha nafsi, inazitia mwangaza nyoyo, kufanya mambo yakapitika na kujaza ulimwengu.

6- Kinachofanya akili ya mwenye busara kuzidi ni kutangamana na watu mfano wake na kujiepusha na walio kinyume chake.

7- Abu Maalik al-Ghazziy amesema:

“Keti na werevu, sawa wawe ni marafiki au maadui. Akili inaipa mwanga akili.”

8- Kutangamana na wenye akili kuna maana mbili. Mosi ni kujikumbusha kitu ambacho yule mwenye busara anakihitajia. Pili ni kuzinduka na kitu cha khatari ambacho mjinga anapaswa kukitambua.

9- Kuwa karibu na mwenye akili ni faida kwa mtu mfano wake na ni mazingatio kwa mtu kinyume chake. Hili linahusiana na hali zote. Haifai kwake akamdhalilikia isipokuwa yule awezae kumdhalilikia. Asiwaendee isipokuwa wale wanaowapenda awaendee.

10- Lau akili ingelikuwa na wazazi basi mmoja wao angelikuwa ni subira na mwengine alikuwa ni kuthibitisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 24-26
  • Imechapishwa: 12/11/2016