Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Wa kwanza wao ni Nuuh (´alayhis-Salaam).

MAELEZO

Haya ndio maoni ya haki. Hakukutumwa kabla ya Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Mtume yoyote. Hapa tunapata kutambua kosa la wanahistoria ambao wanasema kuwa Idriys (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa kabla ya Nuuh. Allaah (Ta´ala) anasema:

إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ

“Hakika Tumekufunulia Wahy kama Tulivyomfunulia Wahy Nuuh na Manabii baada yake.” (04:163)

Katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy imepokelewa kupitia Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) kuhusu uombezi:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa watu wataenda kwa Aadam ili awaombee. Ataomba udhuru na kuwaambia: “Nendeni kwa Nuuh. Hakika yeye ndiye Mtume wa kwanza ambaye Allaah aliwatumia watu wa kwenye ardhi.”

Kwa mujibu wa Qur-aan, Sunnah na maafikiano Nuuh ndio Mtume wa kwanza.

Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio mmoja katika wale Mitume watano bora ambao waliokuwa na subira sana. Nao ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Ibraahiym, Muusa, Nuuh na ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Allaah (Ta´ala) amewataja sehemu mbili katika Qur-aan. Sehemu ya kwanza ni katika Suurah “al-Ahzaab” na ya pili ni katika Suurah “ash-Shuuraa.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Utaymiyn
  • Mfasiri: Fitqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 23/04/2022