05- Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiswali usiku mrefu kwa kusimama na akiswali usiku mrefu kwa kukaa. Alikuwa anaposoma kwa kukaa, anafanya Rukuu´ kwa kukaa, na anaposoma kwa kusimama, anafanya Rukuu´ kwa kusimama[1].
Wakati mwingine alikuwa akiswali kwa kukaa na hivyo anasoma hali ya kukaa. Kunapobaki katika kisomo chake kiasi cha Aayah thelathini au arubaini, anasimama na kuzisoma hali ya kusimama. Halafu anarukuu na kusujudu kisha anafanya vivyo hivyo katika Raka´ah ya pili[2].
Mwishoni mwa uhai wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali swalah ya sunnah kwa kukaa. Hilo lilikuwa mwaka mmoja kabla ya kufa[3].
Alikuwa akikaa kwa kukunja miguu[4].
[1] Muslim na Abuu Daawuud.
[2] al-Bukhaariy na Muslim.
[3] Muslim na Ahmad.
[4] an-Nasaa’iy, Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” yake (1/107/2), ´Abdul-Ghaniy al-Maqdisiy katika ”as-Sunan” (1/80) na al-Haakim ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy ameafikiana naye.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 79-80
- Imechapishwa: 08/10/2016
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
14. Nguzo ya kwanza ya swalah
Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: Nguzo ya kwanza ni kusimama kwa mwenye kuweza. Dalili ni Kauli Yake (Ta ´ala): حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ ”Zichungeni swalah na khaswa khaswa swalah ya katikati na simameni mbele ya Allaah hali ya kuwa ni wanyenyekevu.”[1] MAELEZO…
In "ash-Sharh al-Mumtaaz - Ibn Baaz"
Ameswali ndani ya ndege kwa kukaa ilihali anaweza kusimama
Swali: Niliswali ndani ya ndege kwa kukaa chini pamoja na kujua kwamba naweza kusimama na nafasi ipo. Je, niirudi swalah yangu? Jibu: Ndio. Ni lazima kwako kuirudi swalah yako ikiwa ulikuwa unaweza kusimama. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Imraan bin Huswyan: “Swali kwa kusimama, ikiwa huwezi kwa…
In "Hali ya kusimama"
32. Nguzo ya kwanza ya swalah: Kusimama kwa anayeweza
Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: Nguzo ya kwanza ni kusimama kwa mwenye kuweza. Dalili ni Kauli Yake (Ta ´ala): حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ ”Zichungeni swalah na khaswa khaswa swalah ya katikati na simameni mbele ya Allaah hali ya kuwa ni wanyenyekevu.”[1] MAELEZO…
In "Sharh Shuruwt-is-Swalaah - ar-Raajihiy"