7 – Hali ya jamii
Hapa Qur-aan imemponya mgonjwa na kuangaza njia. Tazama inavyomuamrisha yule kiongozi mkubwa kuiangalia jamii yake:
وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ
“Na inamisha ubawa wako kwa anayekufuata miongoni mwa waumini.”[1]
فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ
“Basi ni kwa sababu ya rehema kutoka kwa Allaah umekuwa mpole kwao na lau ungelikuwa mkali, mwenye moyo mgumu, basi wangelikukimbia. Basi wasamehe na waombee msamaha na washauri katika mambo.”[2]
Tazama namna inavyosema kuiambia jamii ifanye nini na watawala wake:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ
“Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wale wenye madaraka katika nyinyi.”[3]
Tazama inavyosema kumwambia mtu anachotakiwa kufanya na jamaa zake kama mfano wa watoto na mke:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ
“Enyi mlioamini! Jikingeni nafsi zenu na familia zenu kutokana na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali na wenye nguvu hawamuasi Allaah kwa yale anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa.”[4]
Tazama namna inavyomuamrisha mtu awe kwa jamaa zake na kwamba anatakiwa kusamehe na kupuuza endapo watafanya kitu kisichokuwa na uzito. Kwanza inamwamrisha awe ni mwenye kujihadhari baada ya hapo apuuze na kusamehe:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ ۚ وَإِن تَعْفُوا وَتَصْفَحُوا وَتَغْفِرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
“Enyi mlioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na wana wenu [kuna ambao] ni maadui kwenu, basi tahadharini nao! Iwapo mtasamehe na mkapuuza na mkayafutilia mbali, basi hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[5]
Tazama inavyomuamrisha mtu binafsi katika jamii namna wanavyotakiwa kutaamiliana:
إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ
“Hakika Allaah anaamrishia uadilifu na wema na kuwapa [mahitajio na msaada] ndugu wa karibu na anakataza machafu na maovu na dhuluma. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumbuka.”[6]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ ۖ وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا
“Enyi mlioamini! Jieupusheni sana kuwa na dhana [mbaya], kwani hakika baadhi ya dhana ni dhamb, na wala msipelelezane na wala wasisengenyane baadhi yenu wengine.”[7]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ ۖ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ ۖبِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ ۚ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ
“Enyi mlioamini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao – huenda wakawa bora kuliko wao – na wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao – huenda wakawa bora kuliko wao, na wala msikashifianeni na wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ubaya ulioje kutumia jina la ufasiki baada ya kwishaamini. Na yeyote asiyetubu, basi hao ndio madhalimu.”[8]
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ
“Saidianeni katika wema na kumcha Allaah na wala msisaidiane katika dhambi na uadui.”[9]
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ
“Hakika waumini ni ndugu.”[10]
وَأَمْرُهُمْ شُورَىٰ بَيْنَهُمْ
“Na jambo lao hushauriana baina yao.”[11]
Pale ilipokuwa jamii haiwezi kuepuka vikwazo na vipingamizi na wanahitaji dawa ya kutibu maradhi haya yaliyoenea, ndipo akabainisha (Ta´ala) dawa sehemu tatu katika Kitabu Chake. Kikwazo cha mtu kinatibiwa kwa njia ya kwamba mtu asirudishe ubaya uleule kwa yule aliyemfanyizia. Badala yake mtu anatakiwa kulikabili tatizo hilo kwa kutangamana naye kwa uzuri. Ama kuhusu majini, mtu anaweza kujikinga nayo kwa kumuomba Allaah kinga kutokamana na wao.
Sehemu ya kwanza: Ameeleza (Ta´ala) dawa dhidi ya kikwazo cha mwanaadamu mwishoni mwa Suurah “al-A´raaf” na kusema:
خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ
“Shikamana na usamehevu na amrisha mema na jiepushe na wajinga.”[12]
Kuhusu vikwazo vya majini amesema:
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۚ إِنَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
“Na pindi utakapokuchochea uchochezi kutokana na shaytwaan, basi jikinge na Allaah. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na ni mjuzi.”[13]
Sehemu ya pili: Katika Suurah “al-Mu´minuun” amesema kuhusu kikwazo cha mwanaadamu:
ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ السَّيِّئَةَ ۚ نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَصِفُونَ
“Ondosha maovu kwa njia [ya kufanya] yale yaliyo mema zaidi. Sisi Tunajua zaidi yale wanayoyaelezea.”[14]
Upande mwigine amesema kuhusu majini:
وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ
“Sema: “Mola wangu! Najikinga Kwako kutokana na uchochezi wa mashaytwaan na najikinga Kwako Mola wasinihudhurie.””[15]
Sehemu ya tatu: Katika Suurah “Fuswswilat” amebainisha (Ta´ala) zaidi ya kwamba dawa hii ya kimbingu inaponya maradhi haya ya kishaytwaan. Kadhalika akabainisha kuwa sio kila mtu anapata dawa hii ya kimbingu. Hakuna mwenye kuipata isipokuwa tu yule mwenye fungu na bahati kubwa. Amesema kuhusu hilo katika Aayah ifuatayo:
وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ۚ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ
“Na wala haulingani sawa wema na uovu. Lipiza [uovu ulilotendewa] kwa ambalo ni zuri zaidi; tahamaki yule ambaye baina yako na baina yake kuna uadui atakuwa kama ni rafiki wa ndani. Hawatopewa sifa hii isipokuwa wale waliovuta subira na hapewi hayo isipokuwa mwenye fungu kubwa.”[16]
Kuhusu kikwazo cha shaytwaan amesema:
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
“Na utakapokuchochea uchochezi kutoka kwa shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi.”[17]
Sehemu nyingine amebainisha kuwa upole na ulaini huu inahusiana tu na muumini na si kafiri. Amesema:
فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ
“… basi Allaah atawaleta watu [badala yao] atakaowapenda nao watampenda, wanyenyekevu kwa waumini, washupavu kwa makafiri.”[18]
مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ
“Muhammad ni Mtume wa Allaah na wale walio pamoja naye ni washupavu zaidi kwa makafiri; wanahurumiana kati yao.”[19]
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ
“Ee Nabii! Pambana jihaad na makafiri na wanafiki na kuwa mgumu kwao.”[20]
Kuweka ukali mahali kunatakiwa upole, ni upumbavu na uzembe. Kuweka upole mahali kunatakiwa ukali, ni udhaifu na kutoweza.
Kunaposemwa ´upole`, sema kuwa upole una nafasi yake
Upole wa kijana isipokuwa nafasi yake ni ujinga
[1] 26:215
[2] 03:159
[3] 04:59
[4] 66:06
[5] 64:14
[6] 16:90
[7] 49:12
[8] 49:11
[9] 05:02
[10] 49:10
[11] 42:38
[12] 07:199
[13] 07:200
[14] 23:96
[15] 23:97-98
[16] 41:34-35
[17] 41:36
[18] 05:54
[19] 48:29
[20] 09:73
- Mhusika: Imaam Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Islaam diyn al-Kaamil, uk. 16-18
- Imechapishwa: 13/06/2023

Mhusika: Imaam Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Islaam diyn al-Kaamil, uk. 16-18
Imechapishwa: 13/06/2023
https://firqatunnajia.com/05-hali-ya-jamii/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)