05. Hadiyth “Yule mwenye kutawadha na akatia vizuri wudhuu´ wake… “

230 – Abud-Dardaa´ amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَن توضأَ فأحسن الوضوء، ثم قام فصلّى ركعتين أو أربعاً -يشك سهل- يُحسِنُ فيهنَّ الذِّكرَ والخشوع، ثم استغفر اللهَ؛ غَفَر له

“Yule mwenye kutawadha na akatia vizuri wudhuu´ wake kisha akasimama na kuswali Rak´ah mbili au nne – Sahl ametia shaka –  ambapo akafanya vizuri dhikr na unyenyekevu ndani yake halafu akamuomba Allaah msamaha, basi Allaah atamsamehe.”[1]

Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi nuzri.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/211)
  • Imechapishwa: 29/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy