05. Hadiyth ” Naapa kwa Allaah mtazisawazisha safu zenu au Allaah… ”

15 – an-Nu’maan bin Bashiyr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwageuzia watu uso wake na kusema:

“Zisawazisheni safu zenu, zisawazisheni safu zenu, zisawazisheni safu zenu. Naapa kwa Allaah mtazisawazisha safu zenu au Allaah atafanya migongano kati ya nyoyo zenu.” Amesema: “Kisha nikamuona mtu akiegemeza bega lake na bega la mwenzake, goti lake na goti la mwenzake na kifundo cha mguu wake na kifundo cha mguu wa mwenzake.”[1]

16 – Abu Hurayra (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwageuzia watu uso wake na kusema:

”Fanyeni uzuri kunyoosha safu ndani ya swalah.”[2]

17 – Abu Sa’iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”…pindi mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi nyoosheni safu zenu, zifanyeni sawa na zijazeni mapengo; kwani mimi naona nyuma yangu…”[3]

18 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”.. zibeni mapengo.”[4]

[1] Abu Daawuud (662) na Ibn Hibbaan (2173) kwa ukaguzi wa al-Albaaniy.

Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud.” Angalia pia “as-Silsilah as-Swahiyhah” ya al-Albaaniy (32).

[2] Ahmad na Ibn Hibbaan (2176) kwa ukaguzi wa al-Albaaniy ambaye ameisahihisha. Ameisahihisha tena katika “Swahiyh al-Targhiyb” (499).

[3] Ahmad (11007), Abu Ya’laa (1355), Ibn Abiy Shaybah (3819), Ibn Khuzaymah (1548) na Ibn Hibbaan (402) kwa ukaguzi wa Shu’ayb (403) na kwa ukaguzi wa al-Albaaniy.

Ni Swahiyh kwa mujibu wa Shu’ayb katika maelezo yake ya “al-Musnad” na ya “Swahiyh Ibn Hibbaan.” Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika maelezo yake ya “Swahiyh Ibn Hibbaan.”

[4] Abu Daawuud (681). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abu Daawuud” (632).

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ujuwb Taswiyat-is-Sufuuf
  • Imechapishwa: 22/01/2025